• Ajira
  • Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala ya Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Bodi ya Ushauri
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • Watumishi wa Umma Mkoani Mbeya wavutiwa na Mradi wa Nyumba Bunju

    3 months ago
  • Wengi wavutiwa na Banda la TBA Nanenane Simiyu

    5 months ago
  • TBA yashiriki Maonyesho ya Nanenane

    5 months ago
  • TBA yapata Tuzo katika Maonyesho ya 42 ya Sabasaba

    5 months ago

Latest Press Release

  • Wapangaji Nyumba za Wakala wa Majengo Tanz... Jan 29, 2019

  • Taarifa kwa vyombo vya habari

    Dec 04, 2017

Kurugenzi ya Miliki

UTANGULIZI

Idara ya Miliki ni kati ya Idara kuu tatu zilizopo chini ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae anasaidiwa kusimamia na kutekeleza majukumu ya Idara kwa ushirikiano wa kitengo cha Usimamizi na Uendeshaji wa Miliki ya nyumba za Wakala, Kitengo kingine ni cha Utafiti na Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania. Aidha, ipo sehemu inayoshughulika na kuweka kumbukumbu za mikataba ya mauzo ya nyumba za Serikali.

Vitengo hivi vinaongozwa na wakuu wafuatao;

i. Msimamizi wa Nyumba - Chief Property Manager

ii. Msimamizi wa Utafiti na miradi ya Maendeleo Chief Research and Planning Development Manager.

iii. Msimamizi wa sehemu ya utunzaji wa kumbukumbu za miliki ya Serikali (Data Base Documentalist)

MAJUKUMU YA IDARA

Idara ya Miliki ina majukumu yafuatayo:

i. Kuhakikisha Wakala unamiliki maeneo kwa ajili ya ujenzi wa majengo na nyumba za watumishi wa umma.

ii. Ujenzi wa nyumba mpya za Serikali

iii. Uuzaji wa nyumba za Serikali kwa watumishi wa umma.

iv. Upangishaji wa nyumba za Serikali kwa viongozi na watumishi wa umma.

v. Uwekaji samani kwenye nyumba za Viongozi

vi. Upangishaji wa baadhi ya nyumba za Serikali kibiashara.

vii. Matengenezo ya nyumba/majengo ya Serikali.

viii. Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusiana na masuala yanayohusu nyumba na usimamizi wa Miliki.

ix. Kutoa huduma ya usimamizi wa matumizi ya majengo ya Serikali yaliyokwisha kukamilika (Facility Management).

MAJUKUMU YA KITENGO CHA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA NYUMBA

Kitengo cha usimamizi na uendeshaji wa milikikina majukumu ya kusimamia nyumba za viongozi, upangishaji wa nyumba kwa watumishi wa Serikali, kibiashara pamoja na uendeshaji wa nyumba hizo. Kitengo hiki pia kinasimamia matengenezo ya nyumba za Wakala.

MAJUKUMU

YA KITENGO CHA UTAFITI NA MIRADI

Kitengo cha cha utafiti na miradi kina jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa viwanja pamoja na miliki zake kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Wakala. Kuandaa uchambuzi yakinifu wa ndani kwa miradi ya maendeleo ya wakala. Kusimamia nyumba/majengo yote yanayorejeshwa Serikalini chini ya wakala na majengo na viwanja vyote yanayomilikwa na Wakala na kusimamia uuzaji wa nyumba za Wakala.

Aidha, kitengo hiki kinatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uthamini wa majengo na Ardhi ya Serikali

MAJUKUMU YA SEHEMU YA DATA BASE

Sehemu hii (Section) inasimamia uwekaji kumbukumbu

sahihi ya miliki ya Serikali ikiwa ni pamoja na nyumba zinazouzwa na kupangishwa

nchi nzima, viwanja na maeneo ya Serikali yaliyonunuliwa.


Tanzania Buildings Agency
Opposite karimjee Hall,P.O.Box 9542 Dar es Salaam Tanzania
Nukushi : +255 22 2114143
Namba ya Simu : +255 22 2122163/ 2117114
Barua Pepe : ce@tba.go.tz/ info@tba.go.tz

Linki za Haraka

  • Nyumba Zinazouzwa
  • Mpango Mkakati wa 2012-2017
  • Vipeperushi
  • Kanuni
  • Sheria

Linki Linganifu

  • Tume ya Ajira
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Utumishi
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
  • Sera ya Faragha
  • Mikatazo
  • Maswali
  • Ramani Ya Tovuti
  • Staff Mail

©2019 wakala ya majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Wakala ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania